You are currently viewing Nicah The Queen afungua kesi dhidi ya Emma Jalamo

Nicah The Queen afungua kesi dhidi ya Emma Jalamo

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Nicah the Queen ameamua kumchukulia hatua kali za kisheria msanii wa ohangala Emma Jalamo kwa tuhuma za kuichafu brand yake ya muziki.

Kupitia barua ya mawakili wake, Nicah ametoa makataa ya siku saba kwa Jalamo kutumia mtandao wake wa kijamii wa Facebook kuomba msamaha kwa kujaribu kuvunja ndoa yake, la sivyo ajiandae kukutana naye kortini.

Hii ni baada ya mapema wiki hii Nicah kuibuka na kumsuta vikali Jalamo kwa madai ya kuisambaratisha ndoa yake lakini pia kitendo cha kumtumia pesa na kumu-posti kwenye ukurasa wake wa Facebook bila ridhaa yake.

Jambo ambalo anadai lillimfanya mwanaume wake kumkimbia baada ya kushuku kuwa huenda anatoka kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Hata hivyo kitendo hicho kilizua hisia mseto miongoni mwa walimwengu mtandaoni ambapo wengi walienda mbali zaidi na kuhoji kuwa huenda mrembo huyo anatumia sakata hilo kutangaza wimbo wake mpya na Jalamo, madai ambayo alijitenga nayo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke