You are currently viewing NICAH THE QUEEN NA AMBER RAY WAINGIA KWENYE BIFU KISA WANAUME

NICAH THE QUEEN NA AMBER RAY WAINGIA KWENYE BIFU KISA WANAUME

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Niccah The Queen amezua mjadala mzito mtandaoni mara baada ya kumchana soshalaiti maarufu nchini Amber Ray kupitia ujumbe wake aliokuwa anatoa rai kwa wanawake wenzake kuwaombea waume zao kutokana na majaribu wanayokumbana nayo maishani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nicah The Queen amesema kwamba hana ugomvi wowote na Amber Ray na hatumia jina lake kutafuta kiki kama inavyotafsiriwa mtandaoni ila alikuwa anawahimiza wanawake kuwaombea waume zao kutokana na majaribu ambayo wanawake wenzao huwapa wanapokuwa wanatafuta riziki.

Kauli ya nicah the Queen haijapokolewa vyema na Amber Ray ambaye ameamua kumjibu Nicah The Queen kwa kejeli kupitia instastory yake kwa kusema kwamba uzembe wake wa kujificha kwenye maombi ndio ulipelekea ndoa yake na Dr. Ofweneke kuvunjika, jambo lilopelekea wanawake wenye bidii kunyanganya mume.

Hata hivyo watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wamehoji kuwa wawili hao wamehamua kuingia kwenye bifu ya uongo kwa ajili ya kutangaza project yao mpya

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke