You are currently viewing NICCAH THE QUEEN AMKINGIA KIFUA WILLY PAUL

NICCAH THE QUEEN AMKINGIA KIFUA WILLY PAUL

Aliyekuwa mke wa Dr. Ofweneke msanii Niccah the Queen amejitokeza hadharani na kumkingia kifua nyota wa muziki nchini Willy Paul baada ya Diana Marua kudai kwamba Bosi huyo Saldido alijaribu kumbaka.

Kupitia  instagram live mrembo huyo amesikitisha na hatua ya   Diana Marua kudanganya kuwa alibakwa na Willy Paul ikizingatiwa kuwa kipindi hicho wawili hao  walikuwa wapenzi.

Niccah ambaye alikuwa anaishi katika mjengo wa kifahari wa Great Wall Apartment akiwa bado yupo kwenye ndoa na Dr. Ofweneke ameeleza kuwa alikuwa kwenye eneo la tukio wakati Diana alikuwa ndani ya gari ya Willy Paul huku akiwa amekaa bila uwoga wowote.

Hata hivyo amemtaka Diana Marua amwambie mume wake Bahati ukweli badala ya kumbambikia Willy Paul tuhuma za uongo ambazo kwa mujibu wake huenda ikamsababishia msanii huyo tatizo la afya ya akili. 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke