You are currently viewing NICAH THE QUEEN AWAPA SOMO WANAWAKE KUHUSU UTARATIBU WA ULEZI WA PAMOJA KWA WATOTO (CO-PARENTING)

NICAH THE QUEEN AWAPA SOMO WANAWAKE KUHUSU UTARATIBU WA ULEZI WA PAMOJA KWA WATOTO (CO-PARENTING)

Female singer kutoka Kenya Nicah The Queen ametoa changamoto kwa wanawake wenzake kujishusha na kushirikiana na wapenzi wao wa zamani kuwalea watoto wao waliozaa nje ya ndoa badala ya kuendekeza kiburi na majivuno.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nicah The Queen amesema kiburi na majivuno imewaponza wanawake wengi na kuwafanya kuona utaratibu ulezi wa pamoja yaani, Co-parenting kuwa mgumu kwao jambo ambalo anadai limepelekea watoto wengi kukosa upendo wa baba katika maisha.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Na Wewe” amesema kila mtoto ana haki ya kupata upendo na mahitaji ya msingi kutoka kwa mama na baba mzazi licha ya utofauti wao.

Kauli ya Nicah The Queen imekuja mara baada ya kukutana baby daddy wake Dr. Ofweneke kwenye hafla ya kufuzu kwa mtoto wao ambapo walimuonyesha upendo licha ya kutengana na kuingia kwenye mahusiano mengine tofauti.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke