Ni miaka 8 imepita tangu ndoa yao ivunjike lakini Nick Cannon bado analikumbuka penzi lake na Mariah Carey.
Kwenye mahojiano na Podcast ya The Hottee Talk Show, Cannon amesema hatoweza kuwa na upendo tena kama aliowahi kuwa nao akiwa na Mariah Carey.
Aidha ameongeza kwa kusema, anaweza kurudiana na Mariah Carey kama mambo yatakuwa kama yalivyokuwa.
Wawili hao walifahamiana mwaka 2005 lakini walianza mahusiano mwaka 2008, mwaka ambao pia walifunga ndoa.
Ndoa hiyo ilivunjika mwaka 2014 lakini kwa pamoja wana watoto wawili mapacha, Moroccan na Monroe wenye umri wa miaka 11.