Rapa kutoka Marekani Nicki Minaj amemfungulia mashtaka mtengeneza maudhui ya YouTube (Marley Green) maarufu kama Nosey Heaux mara baada ya kuibua madai kuwa rapa huyo anatumia dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, Nicki Minaj amedai Nosey alipakia video hiyo juzi Jumatatu na kumchafua kwa shutuma hizo ikiwemo pia kumtaja mtoto wake wa kiume kwamba atakuwa mbakaji kama baba yake, Kenny Petty.
Minaj amedai fidia ya zaidi ya Shillingi Millioni 9 za Kenya lakini pia ametishia kulichukua Jina la ‘Nosey Heaux’ ambalo linatumika kibiashara, kama mwanadada huyo blogger akishindwa kulipa pesa hizo. Nicki Minaj pia ameweka wazi msimamo wake kwamba yeyote ambaye atasambaza habari za uwongo kumuhusu basi atawajibishwa.