Malkia wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani Nicki Minaj amemfikia Rihanna kwa idadi ya video ambazo zimefikisha Jumla ya views Bilioni 1 kwenye mtandao wa YouTube.
Minaj amefikisha video 8, sawa na Rihanna. Rapa huyo amefikia hatua hiyo kupitia video aliyoshirikishwa na Justin Bieber “Beauty And A Beat” ambayo pia inamfanya Justin Bieber kufikisha video 11 zenye idadi hiyo ya watazamaji.