You are currently viewing Nikita Kering aachia rasmi EP yake mpya

Nikita Kering aachia rasmi EP yake mpya

Mwanamuziki kutoka Kenya Nikita Kering ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la The Other Side.

EP hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki ina jumla ya ngoma sita za moto ambazo amezifanya bila kumshirikisha msanii yeyote.

The Other Side EP ina ngoma kama Save Me, Get Through, Fallling Down, Unrelatable, Love Outside, On Yah na inapatikana exclusive kwenye majukwaa yote a kupakua na kusikiliza muziki mitandaoni.

Hii ni EP ya pili kwa mtu mzima Nikita Kering baada ya A Side of Me iliyotoka mwaka 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju saba ya moto.

Utakumbuka juzi kati Nikita Kering’ alisaini mkataba wa Ubalozi na mtandao wa kusikiliza muziki wa Spotify kupitia mpango wa muziki uitwao EQUAL.

EQUAL ni mradi ambao unalenga kuleta usawa wa kijinsia kwenye muziki lakini pia kuwasaidia wasanii wa kike na watengeneza maudhui katika mitandao kijamii kutanua wigo wa kazi zao ili iwafikie watu wengi duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke