You are currently viewing Nikita Kering alamba shavu la ubalozi Spotify

Nikita Kering alamba shavu la ubalozi Spotify

Mwimbaji wa RNB na Pop kutoka Kenya Nikita Kering’ anazidi kuchana mbuga kimataifa mara baada ya kusaini mkataba wa Ubalozi na mtandao wa kusikiliza muziki wa Spotify.

Nikita ametangazwa kuwa balozi wa mpango wa muziki uitwao EQUAL ambao unaendeshwa na mtandao wa kustream muziki  wa spotify kwa mwezi wa Novemba.

Mrembo huyo ambaye yupo mbioni kuachia EP yake mpya anajiunga na orodhaa ya wasanii wa kike kutoka Afrika ambao wamewahi kuwa mabalozi mpango huo hapo awali.

Wanamuziki wengine wa kike kutoka nchini Kenya ambao hapo awali walitajwa kuwa mabalozi wa mpango wa EQUAL ni pamoja na Muthoni Drummer Queen na Sylvia Ssaru.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Spotify wamechapisha habari iliyosomeka “There’s nothing #Unrelatable about November’s #EQUALAfrica ambassador @nikita_kering  Listen to all the incredible voices of #EQUALAfrica at the link in bio.”

EQUAL ni mradi ambao unalenga kuleta usawa wa kijinsia kwenye muziki lakini pia kuwasaidia wasanii wa kike na watengeneza maudhui katika mitandao kijamii kutanua wigo wa kazi zao ili iwafikie watu wengi duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke