You are currently viewing NIKITA KERING ASHINDA TUZO AFRIMMA 2021

NIKITA KERING ASHINDA TUZO AFRIMMA 2021

Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2021 limehitimishwa usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria katika Hoteli ya Eko.

Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Eddy Kenzo, Fally Ipupa, Mr Flavour na wengineo.

Kenya tumetoka kimasomaso kwenye hafla ya tuzo hizo kupitia Nikita Kering ambaye ameshinda katika kipengele cha “Best Female Artist East Africa”  na “Best Artist RnB & Soul.”

Nikita Kering amewashinda wakali kama Rema Namakula, Nandy, Spice Diana, Zuchu, Rosa Ree,Xeniah Manaseh,Karun pamoja na Merry Zerabruk.

Sauti Sol wameibuka washindi kupitia kipingele cha Best group huku msanii chipukizi nchini Shanah Manjeru akishinda kipengele cha Best African Female Artiste

Tuzo za Afrima ambazo zilianza kutolewa tangu mwaka 2015, wawakilishi wengine kutoka Kenya waliokuwa wanawania mwaka huu ni pamoja na Nviiri the story teller, Sauti sol, Nadia Mukami, Khaligraph jones, Tanasha donna, Otile Brown, Xeniah Manaseh, na Muthoni the drummer Queen

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke