Wasanii wa Bongofleva Diamond Platnumz, Harmonize na Zuchu wamechaguliwa kuwania tuzo za “The Headies” ambazo ni tuzo kubwa za nchini Nigeria.
Watatu hao wapo katika kipengele kimoja cha Msanii Bora Afrika Mashariki, huku Diamond akiwania kingine cha Msanii Bora wa Mwaka Afrika.
Kwenye kipengele cha Msanii Bora Afrika Mashariki, watatu hao wanachuana na Meddy (Rwanda), Nikita Kering (Kenya) na Eddy Kenzo (Uganda).
Kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka Afrika, Diamond Platnumz anachuana na Davido, Burna Boy, Wizkid (Nigeria), Aya Nakamura (Mali), Black Coffee (Afrika Kusini) na Soolking (Algeria) kwenye kipengele hicho.
Tuzo hizo za 15 mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Septemba 4, huko Atlanta nchini Marekani.