Hatimaye Rapa kutoka nchini Tanzania Nikki Mbishi ameachia rasmi album yake mpya aliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki zake.
Hitmaker huyo “Babu Talent” amewabarki mashabiki zake na ‘Welcome to Gamboshi’ album ambayo ina jumla ya nyimbo 22 za moto, ikiwa na kolabo 12 kutoka kwa wakali kama Ally Choki, P Mawenge, Wakazi, Tk Ndendezi, Zaiid pamoja na wengine wengi.
Album hiyo kwa sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya ku-stream muziki duniani na ina ngoma kama Welcome to Gambosh, Party ya Uwaki, Wazee Wabishi, Wanyonge, Nenda na nyingine nyingine.
Album ya “Welcome to Gamboshi” inazifuata album kama Sauti ya Jogoo, Ufunuo wa unju na Sam Magoli kutoka kwa mtu mzima Nikki Mbishi.
.