You are currently viewing NIKKI MBISHI:  MARIOO ALISTAHILI KUPEWA MIRABAHA NA COSOTA KUTOKA KAZI ZAKE KUPIGWA SANA KWENYE MEDIA

NIKKI MBISHI: MARIOO ALISTAHILI KUPEWA MIRABAHA NA COSOTA KUTOKA KAZI ZAKE KUPIGWA SANA KWENYE MEDIA

Rapa kutoka nchini Tanzania Nikki Mbishi amesema Marioo kupitia wimbo wake “BIA TAMU” alistahili kuwa namba moja kwenye orodha ya wasanii ambao wamepata gawio la mirabaha kutoka Chama cha Hatimiliki Tanzania – COSOTA.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nikki mbishi amesema wimbo wa Bia Tamu umepigwa kuliko wimbo wowote nchini Tanzania katika kipindi cha miezi 7 iliyopita.

“Yaani mtu unakuja na hoja jenzi ambayo pengine ingewapa hamasa Con Boi na Rapcha watu wanahisi umewalinganisha. Jamaa wapo kama COSOTA wakiulizwa vigezo vya kutoa mirabaha, hata mjinga anajua MARIOO alistahili kuwa namba moja BIA TAMU imepigwa kulizo nyimbo zote kwa 7 months ago.” alichomekea Nikki Mbishi wakati akichangia hoja kwenye tweet ya Wakazi iliyoibua mjadala mzito Twitter, tangu juzi.

Kwa mujibu wa COSOTA,  Ali Kiba ndiye aliongoza kwa wasanii wa bongo fleva waliopata pesa nyingi za Mirabaha ambapo alipata kiasi cha shilling 3 za Kenya huku Marioo akikosekana hata kwenye TOP 20 ya orodha hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke