You are currently viewing Nilitabiri Spice Diana atapata mafanikio makubwa kwenye muziki – Bebe Cool

Nilitabiri Spice Diana atapata mafanikio makubwa kwenye muziki – Bebe Cool

Bosi wa label ya Gagamel, Msanii Bebe Cool anasema alikuwa amemtabiria mema Spice Diana kipindi anatoka kimuziki miaka minane iliyopita.

Bebe Cool amesema alikuwa anajua mrembo huyo atakuwa mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi nchini Uganda bila usaidizi wowote wa staa mkubwa nchini humo.

Aidha amefafanua sababu za kukataa kufanya kolabo na Spice Diana kwa kusema kuwa ilikuwa njia ya kumpa changamoto aendelee kuipambania brand yake hadi atakapoachia wimbo mkali kama msanii wa kujitegemea.

“Miaka minane iliyopita, Spice Diana na meneja wake walikuja kwangu wakiomba kolabo. Tulikutana kwenye baa moja mjini Ntinda. Nilimwambia afanye kazi kwa bidii hadi atakapoachia wimbo mkali bila usaidizi wa mtu yeyote,” Bebe Cool alielezea.

Hata hivyo anaamini ikitokea wamefanya kazi ya pamoja na Spice Diana watafaidi wote kwa kuwa mrembo huyo ameacha alama kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kutokana na nyimbo ambazo amekuwa akiaziachia katika miaka ya karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke