Staa wa muziki nchini uganda Nina Roz anaweza kuwa msanii aliyefanikiwa kutoa hits nyingi tangu aanze safari yake ya muziki, lakini bado anatamani kupata shahada kutoka chuo kikuu.
Katika mahojiano na Galaxy FM, Nina Roz amefunguka na kudai kwamba aliacha shule akiwa mwaka wa pili alipokuwa akisomea shahada ya Business Administration katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Mashariki (IUEA).
Himaker huyo wa “Muliro” amedokeza mpango wa kurudi tena shule ili aweze kutimiza ndoto yake ya kusomea kozi ya digrii katika Chuo Kikuu.
Hata hivyo Nina Roza amesema sababu za kuacha masomo akiwa chuo kikuu zilikuwa nje ya uwezo wake.