Mwanamuziki Eddy Kenzo ameahidi kuwaunganisha wanamuziki wengine wa Uganda na waandaaji wa tuzo za Grammy pindi atakapohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo hizo mwakani nchini marekani.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Kenzo amebainisha kuwa kuteuliwa kwenye tuzo za Grammy 2023 itawafungulia milango wasanii wengi nchini humo kuupeleka muziki wao kimataifa na kushiriki tuzo kubwa duniani .
“Nataka kwenda Marekani na kukutana na watu hawa. Nataka kuwajua ili niweze kuwaunganisha na wanamuziki wa Uganda. Nataka kufungua mlango kwa kila mtu,” alisema Eddy Kenzo.
Eddy Kenzo ametajwa kuwania Tuzo za Grammy mwaka 2023 kupitia kipengele cha Best Global Music Performance na wimbo wake ‘Gimme Love’ aliomshirikisha Matt B.