You are currently viewing NONINI AFUNGUA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA BRIAN MUTINDA

NONINI AFUNGUA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA BRIAN MUTINDA

Mwanamuziki wa Kenya anayeishi Marekani Hubert Nakitare maarufuka kama  “Nonini” amefungulia mashtaka mwanamitandao Brian Mutinda na kampuni ya kieletroniki ya Syinix.

Hii ni baada ya mwanamitandao huyo kutumia wimbo wake wa “We Kamu” kwenye matangazo ya kibiashara kwenye mitandao ya kijamii bila idhini yake.

Kulingana na shtaka hilo lilofunguliwa katika mahakama ya milimani jijini Nairobi, mshatikiwa ametakiwa kufika binafsi  kortini ndani ya siku 15  au akiwa na wakili wake la sivyo hatachukuliwa hatua kali za kisheria.

Utakumbuka mwezi Aprili mwaka huu nonini alitishia kumfungulia mashataka brian mutinda kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake ambapo alitoa nafasi ya mazungumzo kati yake na kampuni ya Syinix na Brian Mutinda lakini inaonekana hatua hiyo haikuzaa matunda yoyote.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke