You are currently viewing NONINI AJIONDOA KAMA MWANACHAMA WA MCSK

NONINI AJIONDOA KAMA MWANACHAMA WA MCSK

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Nonini ametangaza kujiondoa kama mwanachama wa chama cha muziki na hakimiliki nchini MCSK.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nonini amechapisha barua inaonesha kuwa ombi lake kujitoa kama mwanachama wa chama cha muziki na hakimiliki nchini MCSK imekubaliwa huku akithibitisha kuwa hatakuwa anapokea mirabaha ya muziki wake kutoka kwa chama hicho.

“Insanity is doing the same thing over and over and expecting different results. Moving on to something that actually works. 💯 #Mgenge2ru”, Ameandika Instagram.

Mwaka wa 2018 Nonini alijiuzulu kama mwenyekiti wa chama inayopigania haki ya watumbuzaji nchini PRISK kwa kile kilichotajwa kuwa prisk ilikwenda kinyume na kanuni zilizowekwa na bodi ya hakimiliki nchini KECOBO.

PRISK ni chama ambacho kilipewa leseni ya kuhudumu na Bodi ya hakimiliki nchini KECOBO kuhakikisha inatetea maslahi ya wasanii na watumbuizaji kupitia kazi zao za sanaa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke