Mwanamuziki mkongwe Nonini ameikimbia Kenya na kuamua kutafuta mapato ya muziki wake nchini Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa instagram noni ametangaza rasmi kuwa amejiunga na American Society of Composers, Authors and Publishers (ASCAP) Chama kinacholinda Hakimiliki za Waandishi wa nyimbo na Watayarishaji kikiwa na zaidi ya memba 850,000.
Nonini amekuwa akiishi nchini Marekani ambapo alianzisha biashara yake ya viatu, mavazi na saa za mkononi.
Wiki iliyopita alitangaza kujivua Uanachama wa Chama cha Hakimiliki ya Muziki nchini Kenya (MCSK) kwa madai ya kutoridhishwa na utenda kazi wake katika mgao wa mirabaha kwa wasanii.