Msanii mkongwe nchini Nonini ametangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa kesi yake dhidi ya Kampuni moja ya Kijapani inayojishughulisha ya uuzaji wa bidhaa za kielektroniki, Synix Electronics.
Nonini ambaye amekuwa Mhubiri wa somo la hakimiliki kwa wasanii wa Kenya, ameweka wazi kuwa tarehe ya kupanda kizimbani na kuanza kucharuana na Kampuni hiyo, ni Machi 23 mwaka huu. Msimamo wake ni kuwa, Hakimiliki itaheshimiwa.
Kampuni hiyo ilitumia sehemu ya wimbo wa Nonini katika matangazo yao ya kibiashara mwaka jana na msanii huyo alidokeza hilo kwa kupakia kipande hicho kwenye ukurasa wake.
Nonini katika malalamishi yake kipindi hicho alisema kuwa, Synix walitumia kipande cha wimbo wake ‘We Kam Tu’ pasi na kupata hakimiliki kutoka kwake.