Rapper wa kike kutoka Kenya Noti flow amefunguka sababu za kuachana na mpenzi wake King alami ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tangu amzawadi na gari mpya.
Kupitia kikao cha maswali na majibu pamoja na mashabiki zake Noti Flow amesema alimvumania King Alami mchana kweupe na mwanaume mzee eneo la runda wakipigana mabusu makali kitu ambacho kilimkasirisha ns kuchukua maamuzi magumu ya kuvunja uhusiano wao.
Wawili hao ambao wanashiriki mapenzi ya jinsia moja wamekuwa wakichumbiana tangu mwaka wa 2021 ambapo walienda mbali zaidi na kuchora tattoo za majina yao kwenye miili yao.