Mwanamuziki mwenye utata nchini Noti Flow amekiri kuumia na kujutia kitendo cha kuvunja mahusiano yake na aliyekuwa mpenzi wake, King Alami.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Noti flow amesema mahusiano yao hayangevunjika huenda tukio la king alami kutaka kujiua kwa kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano alingefanyika.
Aidha amefichua kuwa watu wengi mitandaoni wanamlaumu kuwa yeye ndio chanzo cha kisa hicho kutokea huku akisema kuwa jumbe hizo zimemfanya ajihisi vibaya zaidi kwa hatua ya kumkimbia mrembo huyo ambaye walikuwa wanashiriki pamoja mapenzi ya jinsia moja.
“We gon pray for you my baby We’ve been praying for you day & night . You’re strong my G & you’re still the coolest stud I fell in love with I love you more everyday Nothing’s changed & I’m with you thru it all.. I’m here for you forever my love. Quick recovery my baby you are loved and cherished ( for those who are blaming me thank you very much for making me feel worse & guilty than I already I’m. Y’all are right tho, it’s my fault cz if I was with her she’d be OK & safe like she’s always been so crucify me”. Ameandika
Kauli yake imekuja siku moja baada ya kuwaomba wafuasi wake wamsaidie kuchangisha pesa za kugharamia matibabu ya aliyekuwa mpenzi wake, King Alami ambaye kwa sasa bado amelazwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.