You are currently viewing NOTI FLOW AKIRI KUTESWA NA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA

NOTI FLOW AKIRI KUTESWA NA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KULA

Rapa wa kike nchini Noti flow amefunguka kuhusu tatizo la kiafya ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda sasa.

Kupitia mfululizo wa instastory yake kwenye mtandao wa Instagram mrembo huyo amekiri kuwa amekuwa akipata shida sana kwenye suala la kula chakula, jambo ambalo limemuathiri kiafya kiasi cha kupungua kimwili.

Noti Flow amesema licha ya kupata maelekezo kutoka kwa daktari ya namna ya kukabilia na tatizo hilo, alishindwa kufuata taratibu alizopewa na mhudumu wake wa afya kutokana na yeye kukosa hamu ya kula.

Hata hivyo ameahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha anashirikiana kwa ukaribu na daktari kwa ajili ya kuuweka mwili wake sawa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke