You are currently viewing NOTI FLOW AMPA SOMO MWANAUME ALIYEMUOMBA PENZI KWA SHILLINGI LAKI 2 ZA KENYA

NOTI FLOW AMPA SOMO MWANAUME ALIYEMUOMBA PENZI KWA SHILLINGI LAKI 2 ZA KENYA

Female rapper kutoka Kenya Noti Flow ameonekana kutopendezwa na kitendo cha mwanaume mmoja aliyezama kwenye dm yake na kumuomba penzi kwa Shillingi laki mbili za Kenya.

Kupitia instagram page yake Noti Flow ameshare screen short ya ujumbe aliyotumiwa na mwanaume huyo huku akimpa somo kuwa hana shida ya pesa ikizingatiwa kuwa huwa anatumia kati ya shilling laki 5 hadi million moja kwa wiki.

Hitmaker huyo wa “Foto Moto” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba hatokubali kununuliwa kwa shilling laki 2 huku akiwaonya wanaume wanaomzimia kimapenzi kukoma kumtumia jumbe za mapenzi kwenye mitandao yake ya kijamii kwani ana furaha kwenye mahusiano yake na mrembo King Alami.

Utakumbuka Noti Flow ni moja kati ya wasanii wenye utata nchini kutokana na maamuzi yake ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja na mrembo mwenzake King Alami.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke