You are currently viewing NOTI FLOW AMTAMBULISHA MPENZI WAKE MPYA

NOTI FLOW AMTAMBULISHA MPENZI WAKE MPYA

Mwanamuziki aliyegeukia mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya Noti Flow amemtambulisha mpenzi wake mpya siku chache baada ya kutangaza kuwa yupo single.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram mrembo huyo ameposti video akiwa anajiachia kimahaba na mchumba wake huyo huku akisindikiza na ujumbe unaosomeka “Too hot to stay single. kuingia soko na kutoka”

Huyo anakuwa mpenzi wake wanne ndani ya mwaka huu baada ya jaribio lake la kuingia kwenye mahusiano mengine tofauti kukatishwa na jini mkata kamba.

Hata hivyo walimwengu mitandaoni wameonekana kushangazwa na mienendo ya Noti Flow kukwamilia kwenye mahusiano ya jinsia moja wakati wanaume wapo wengi ambapo wameenda mbali zaidi na kuhoji kuwa huenda mrembo huyo ameshindwa na muziki ndio maana amegeukia mtindo huo wa maisha ambao labda unamuingizia pesa nyingi.

Utakumbuka Noti Flow kwenye moja ya mahojiano yake aliwahi kunukuliwa akisema kwamba hatokuja kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote hadi mwisho wa dunia kwani alipitia kipindi kigumu akiwa na mpenzi wake wa zamani ambaye alimdhulumu kijinsia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke