You are currently viewing NOTI FLOW AMTOLEA UVIVU MUSTAFA

NOTI FLOW AMTOLEA UVIVU MUSTAFA

Siku chache baada ya staa wa muziki nchini Colonel Mustafa kudai kwamba alivunja uhusiano wake wa na Noti Flow mara baada ya mrembo huyo kumuibia akaunti yake ya instagram, sasa Noti Flow amejitokeza na kukanusha madai hayo.

Akiwa kwenye moja ya interview Noti Flow amesema madai hayo haya msingi wowote kwani ni yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumuacha Mustafa baada ya msanii huyo kumvunjia heshima kwa kumsaliti.

Hitmaker huyo wa Foto Moto ameenda mbali zaidi na kumtolea uvivu mustafa kwa kusema kwamba msanii huyo hajui kuandika kiingereza kwa ufasaha na hata wafuasi ambao aliwapata instagram ni kwa sababu ya juhudi zake.

Hata hivyo amesema kama kweli Colonel Mustafa anahisi ana ushawishi mkubwa nchini afungue akaunti nyingine ya mtandao wa instagram aone kama atapata wafuasi wengi.

Ikumbukwe kipindi cha nyuma Noti  Flow alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa Colonel Mustafa lakini mahusiano yao yalikuja yakavunjika kwa kile kilichodaiwa kuwa mrembo huyo alikuwa msumbufu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke