You are currently viewing NOTI FLOW ATAMANI KUWA NA MWANAUME LICHA YA KUSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA

NOTI FLOW ATAMANI KUWA NA MWANAUME LICHA YA KUSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA

Msanii Noti Flow amesema yuko tayari kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume iwapo mchumba wake huyo atamruhusu awe na rafiki wa kike.

Kwenye kikao ya maswali na majibu pamoja na mashabiki katika mtandao wa Instagram mrembo huyo amesema wanawake wengi udanganya kushiriki mapenzi ya jinsia moja ilhali nyuma ya pazia wanatoka kimapenzi na wanaume, kitendo ambacho si cha kingwana.

Noti Flow amesema yeye ni mkweli kwenye suala la mahusiano ya jinsia moja na haoni taabu mwanaume atakayemchumbia akiunga mkono wazo lake la kuwa na mpenzi ambaye ni wa jinsia ya kike.

Utakumbuka Noti Flow baada ya kutambulisha mpenzi wake alitangaza kuachana na mrembo huyo bila kuweka sababu za msingi.

Awali Mrembo huyo alikuwa kwenye mahusiano mengine na King Alami lakini walikuja wakaachana kwa madai ya usaliti kwenye mahusiano yao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke