Rapa Noti Flow ametoa wito kwa mashabiki zake kumuweka kwa maombi mpenzi wake wa zamani King Alami baada ya kudaiwa kuwa alijiangusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano katika barabara ya Lumumba drive jijini nairobi.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Noti Flow ambaye hajathibitisha madai hayo, amewataka walimwengu kuacha kueneza taarifa za uongo mtandaoni na badala yake wamuombee Alami na familia yake kwani kwa sasa wanapitia kipindi kigumu.
Taarifa za King Alami kujiangusha kutoka kwa ghorofa zilitoka jana mara baada ya mtumiaji mmoja wa mitandao wa kijamii kuifahamisha mtandao wa udaku wa Nairobi Gossip kuwa mrembo huyo amekimbizwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta ambako anauguza majeraha mabaya.
” I understand there’s a lot of rumors going around the blog about my X gal. Kindly stop spreading unconfirmed info. The family is kindly requesting for privacy and prayers as we go through this tough time. My heart isbroken & I’m devastated but I’m staying positive and prayerful. Kindly do the same She needs it. I still hope its a dream,” Aliandika Instagram.
Hata hivyo hajajulikana ni kitu gani hasa kilimpelekea King Alami kujirusha kutoka kwa jumba la ghorofa tano ila ni jambo la kusubiriwa.
Utakumbuka juzi kati King Alami alijitokeza kwenye mitandao ya kijamii na kumuomba msamaha Noti Flow waweze kurudiana kwani amelikosa penzi lake baada ya mahusiano yao kuvunjika miezi 6 iliyopita kwa madai ya usaliti.