You are currently viewing NOTI FLOW KUMSHTAKI MPENZI WAKE WA ZAMANI KWA TUHUMU ZA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

NOTI FLOW KUMSHTAKI MPENZI WAKE WA ZAMANI KWA TUHUMU ZA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Msanii wa kike nchini Noti flow amefungulia mashataka aliyekuwa mpenzi wake wa zamani kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Noti Flow amesema licha ya kwamba alimsamehe mpenzi wake huyo, lazima sheria ichukue mkondo wake ikizingatiwa kuwa tayari alikuwa amefungua shauri mahakamani.

Hitmaker huyo “Foto Moto” amesema kwamba yeye kama kielelezo chema kwa vijana wadogo nchini lazima aendelee na kesi hiyo hadi pale haki itakapotendeka ili iwe funzo kwa wanaume wanaoendeleza visa vya kikatili dhidi ya wanawake.

Hata hivyo noti flow amesema jamii inatakiwa kufahamu kuwa vitendo vya kuwadhulumu wanawake vimepitwa na wakati na wanaoendeleza kadhia hiyo wanapaswa kukabiliwa kisheria.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke