You are currently viewing Nuh Mziwanda: nimeshindwa kuachia EP kwa kukosa usimamizi

Nuh Mziwanda: nimeshindwa kuachia EP kwa kukosa usimamizi

Mwanamuziki wa Bongofleva, Nuh Mziwanda ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wasanii kuachana na Lebo zao za muziki wakati wapo wengi wanaotafuta nafasi hiyo na kuikosa.

Nuh ameenda mbali zaidi na kusema kuwa ameshindwa hata kuachia EP (Extended Playlist) yake kutokana na kukosa usimamizi.

“Mimi Nilitangaza Kuachia EP ila Mpaka sasa ishakua BP kwangu mana Kila mtu Ana Mtu wake ‘Nawaonea huruma sana Mnaotoka kwenye Usimamizi “, Ameandika Instagram.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii mbalimbali kuvunja mkataba na lebo zilizokuwa zinawasimamia kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi hazijawekwa wazi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke