You are currently viewing Nviiri the Storyteller alalamikia unyanyapaa dhidi ya watu wenye nywele za rasta

Nviiri the Storyteller alalamikia unyanyapaa dhidi ya watu wenye nywele za rasta

Msanii kutoka nchini Kenya Nviiri the Storyteller amefunguka ubaguzi wanaofanyiwa watu wanaopenda kusuka nywele aina ya dreadlocks katika jamii.

Kupitia waraka mrefu alioundika kupitia ukurasa wake wa Instagram msanii huyo ameonekana kukerwa na kasumba ya watu wenye mitindo ya locks kutengwa kwenye maofisi na maeneo mengine ya umma huku akisema kuwa wafrika wengi wameponzwa na itakidi za wazungu kiasi cha kupoteza asili na kuogopa kuwa sehemu za mila zao.

Msanii huyo wa Sol Generation amesema mtu kusuka nywele au kuvalia mavazi anayopenda haiathiri kivyovyote utendakazi wake kwenye shughuli zao za kila siku kwani ni moja ya kuchangia ukuaji wa tasnia ya ubunifu na mitindo barani Afrika.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa viongozi wa kiafrika kubuniwa kwa kanuni na sera mpya za kuunga mkono tamaduni za kiafrika hasa kwa upande wa mavazi na namna watu wanavyojikwatua.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke