You are currently viewing NYASHINSKI AFUNGA NDOA NA MCHUMBA WAKE ZIA BETT

NYASHINSKI AFUNGA NDOA NA MCHUMBA WAKE ZIA BETT

Baada ya uchumba uliodumu kwa muda, Mkongwe wa muziki nchini Nyashinski amefunga ndoa na Zia Bett.

Ndoa hiyo imefungwa Ijumaa Desemba 10 mwaka 2021 katika Kanisa la Nairobi Chapel kwa siri bila shamrashamra tofauti na ndoa za wasanii mbalimbali nchini ikielezwa kuwa waliohudhuria ni ndugu wachache.

Ndoa hiyo Kikristo ilihudhuriwa na ndugu na marafiki zake wa karibu wakiwemo  Collo, Big Pin,Nameless, DJ Stylez.

Hatua hiyo ya mtu mzima Nyashinski kuasi ukapera imeibua hisia za mashabiki wake na mastaa wenzake ambao wameenda mbali na kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo kubwa maishani.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka 2019, wawili hao walifanya sherehe ya kitamaduni iliyowavutia wengi huko katika Kaunti ya Nandi ambayo ilihudhuriwa na familia, marafiki wa karibu, pamoja na watu mashuhuri kutoka maeneo tofauti tofauti.

Nyanshiski na Zia Bett ni wapenzi wa muda mrefu ambao wamechagua kuyaweka mahusiano yao yaliyodumu kwa kipindi kirefu nje ya umaarufu wao, huku wakiwa wamebarikiwa kupata mtoto mmoja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke