You are currently viewing NYASHINSKI ATANGAZA UJIO WA ONESHO LAKE LA MUZIKI MWEZI APRILI MWAKA 2022

NYASHINSKI ATANGAZA UJIO WA ONESHO LAKE LA MUZIKI MWEZI APRILI MWAKA 2022

Msanii nyota nchini Nyashinski ametangaza kuja na onesho lake liitwalo Shin City ambalo litafanyika mwezi Aprili mwaka huu wa 2022.

Kupitia mitandao yake ya kijamii Nyashinski ametusanua kuhusu ujio wa onesho la Shin City kwa kushare bango la onesho hilo ambalo kwa mujibu wake litafanyika Aprili 16 katika ukumbi wa Burudani wa Carnivore Jijini Nairobi.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Properly” ametoa wito kwa mashabiki zake kuanza kununua tiketi za Show hiyo mapema kupitia wavutia www.tokea.com.

Tangazo la Nyashinski linakuja wiki kadhaa baada ya kudai kuwa ana mpango wa kujenga mji wake nchini Kenya katika siku za hivi karibuni kwenye moja performance yake jambo lilowaacha mashabiki na maswali mengi.

Hata hivyo hatua ya rapa huyo kudai kuwa anakuja mji wake inaonekana kwamba ilikuwa ni njia kuwatangazia mashabiki zake kuhusu ujio wa onesho lake la Shin City.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke