You are currently viewing NYOTA NDOGO AELEZA ANAVYOITWA SURA MBAYA NA WANAUME MITANDAONI

NYOTA NDOGO AELEZA ANAVYOITWA SURA MBAYA NA WANAUME MITANDAONI

Msanii mkongwe kwenye muziki  nchini Nyota Ndogo, amefunguka namna ambavyo amekua akishambuliwa kwa maneno ya kejeli mtandaoni na baadhi ya wanaume kwa kumuita sura mbaya.

Nyota Ndogo kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka namna amekuwa akipokea kejeli haswa kutoka kwa wanaume, baada ya kufikisha umri wa miaka 40 mwaka huu.

“Sasa kuitwa mazee na sura Mbaya nishazoea munaweza mukatafuta maneno makali mengine yakuniita na wengi wao uwa wanaume mybe I look much better at 40 kushinda your galfriend mwenye ako 25.hatukatai uzee uzee ni sunna ni hatizeeki kizembe hatujitupi wall yangu ikikusinya ni block” amesema Nyota Ndogo.

Hata hivyo Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” amesema kwamba amezoea kuitwa sura mbaya na hivyo wanaomshambulia wanapaswa kutafuta maneno mengine ya kumuita huku akieleza kwamba yeye ni mrembo kuliko wapenzi wao wa miaka 25.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke