You are currently viewing NYOTA NDOGO AMSHAMBULIA MWANABLOGU ALIYEMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

NYOTA NDOGO AMSHAMBULIA MWANABLOGU ALIYEMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Nyota Ndogo amechukizwa na kitendo cha mwanablogu mmoja  kuchapisha taarifa za uongo dhidi yake.

Mwanablogu huyo alichapisha taarifa akisema kwamba Nyota Ndogo  alidai kwenye moja ya interview kuwa asipoimba jina lake litazidi kuzungumziwa nchini ikizangatiwa kuwa ni msanii mkongwe ambaye ameacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini.

Sasa kupitia instagram page yake Nyota Ndogo ameibuka na kukanusha madai yaliyoibuliwa na blogger huyo kwa kusema kwamba hajawahi jigamba kuwa yeye ni bora kuliko msanii yeyote kwani hapendi kabisa kujisifu kwenye maisha yake.

Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” amesema kama watu wamechoshwa na muziki wake wa sasa ni afadhali waanze kusapoti biashara yake ya vyakula ya Nyota Ndogo jikoni ambayo makao yake yapo mjini voi, kaunti ya Taita Taveta.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke