Msanii mkongwe nchini Nyota ndogo amethibitisha kulipwa pesa zake siku moja baada ya kudai kuporwa na watu waliotumia vyumba vya kulala katika hoteli yake na kisha kutoroka.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nyota ndogo ameshindwa kuficha furaha yake kwa walioshea video clip akiwa anatoa malalamiko yake ambapo amedai kuwa watu hao walimlipa pesa ya huduma aliyowapa huku wakiomba radhi kwa jaribio la kutaka kumdhulumu jasho lake.
Sanjari na hilo, Msanii huyo amekiri kosa la kuwahudumia watu hao kabla ya malipo huku akiahidi kutorudia makosa yake kwani amejifunza kutoamini watu asiowafahamu.
“Thank you so much my people. Video ya kilio imefika mbali sana jamaa wamelipa na yakutoa.nilikua na number zao but sikueka nilikua na majina Yao but sikueka niliwaurumia juu najua mungewavamia sana,”
“…wameomba pia samahani pia ahsante kwa wote walioshare video ya kiliochangu nyie nyote mumechangia mimi kulipwa. MUNGU awabariki.mumesimama na mimi…pia makosa yetu ni kuwacha waingie kabla kulipa hio kosa sitaikwepa nimekubali pia imenifunza,” Ameandika.