You are currently viewing NYOTA NDOGO: NDOA SIO JELA, UKISHINDWA ONDOKA TU

NYOTA NDOGO: NDOA SIO JELA, UKISHINDWA ONDOKA TU

Msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki nchini Nyota Ndogo amefunguka kuhusu visa vya mauji ambavyo vimeongezeka miongoni mwa wana ndoa katika siku za hivi karibuni.

Kupitia waraka mrefu aliouandika kupitia ukurasa wake wa Instagram Nyota Ndogo amesema kuwa ndoa siyo jela, na mtu akishindwa na masuala ya ndoa anapaswa kuondoka kwani ndoa za siku hizi siyo kama za zamani ambazo mtu anaweza vumilia.

“Wanawake tunavumilia kweli lakini lakini musikubali kuendeshewa ndoa zenu na wazazi wenu. Kweli ndoa nikuvumiliana lakini uvumilivu hio ulikua wakatii wao. Kitambo ilikua hakuna mauwaji ya mke kamuua mume ama mume kamuua mke. Kitambo hapakua na watu sijui kuchomwa na mume mauwaji mpaka Sasa yameingia kwa watoto MUNGU wangu twaelekea wapi?” amesema Nyota Ndogo.

Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” amesema kuwa kama mwanaume hamjali mke wake na anampiga kila wakati ni vyema mwanamke achane nae kwani anaweza kumsababishia matatizo.

“Huwezi kumpiga mke wako Kisha useme unampenda. Vile vile mke pia uwezi kumpiga mume useme unampenda nyinyi mumechokana na nyinyi ndio munajua mulipofikishana. Talaka hairuhusiwi katika dini lakini kwa kikazi hiki unaletewa mwanao maiti ama nimzima lakini Hana viungo vingine vya mwili. Ukinichoka umenichoka hata kuekwe vikao vya nyumba kumi hio ndio haiwezi kua.” amesisitiza Nyota Ndogo.

Nyoa Ndogo ameongeza kuwa “Ifike Mahali tuseme Tosha I will not kill my wife nitamrudisha kwao mzima kama nilivyomchukua atapata mume mwengine na wewe pia utapata mke vile vile kwa mke. INATOSHA JAMANI INATOSHA MAUWAJI YAMEZINI MPAKA HATUOGOPI TENA SIMBA TINAOGOPA MWANADAMU”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke