Nyumba ya nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, marehemu Papa Wemba imefunguliwa rasmi Aprili 24. Nyumba hiyo ilinunuliwa na serikali ya DRC na sasa imekuwa “Hifadhi ya Rhumba”.
Papa Wemba, alianguka na kufariki jukwaani akiwatumbuiza maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan nchini Ivory Coast mnamo mwaka wa 2016.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala, Aprili 24 ametimiza miaka 6 tangu afariki dunia mwaka wa 2016.
Hatua ya DRC kufanya nyumba ya Papa Wemba kuwa Hifadhi ya Rhumba inakuja miezi michache baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kitamaduni kutambua Rhumba ya Congo, na kuipatia hadhi ya kulindwa na Unesco.