You are currently viewing OCTOPIZZO ADOKEZO UJIO WA KOLABO NA NYASHINSKI, ZIARA YAKE YA KIMUZI PAMOJA NA ALBUM MPYA

OCTOPIZZO ADOKEZO UJIO WA KOLABO NA NYASHINSKI, ZIARA YAKE YA KIMUZI PAMOJA NA ALBUM MPYA

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Octopizzo ametangaza ujio wa wimbo wake mpya aliyomshirikisha na lejendari wa muziki Nyashinski

Octopizzo amethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki zake Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare picha akiwa na  Nyashinski  ambapo  amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea collabo yao ambayo kwa mujibu wake itakuwa moto wa kuotea mbali.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Motivation” hajeweka wazi ni lini hasa ngoma hiyo itaingia sokoni ila itakuwa wimbo wake wa kwanza kufanya na  Nyashinski tangu aanze safari yake ya muziki.

Mbali na hayo, Octopizzo ametangaza kuja na ziara ya kimuziki iitwayo live music tour samba na kuachia album mpya ambayo hajataja Siku Rasmi ya kuachia Album hiyo lakini ameweka baadhi ya picha zikimuonesha akiwa kwenye maandalizi ya Album yake Mpya.

Hii  inaenda kuwa Album ya 7 kwa mtu mzima Octopizzo, baada ya  Fuego”  iliyotoka mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 12 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke