You are currently viewing OCTOPIZZO AKIRI KUCHOSHWA NA WANAOMKOSOA MTANDAONI

OCTOPIZZO AKIRI KUCHOSHWA NA WANAOMKOSOA MTANDAONI

Rapa Octopizzo amefunguka sababu za kutowajibu wanaomkosoa kwenye mitandao ya kijamii tofauti na ilivyokuwa awali.

Akipiga stori na presenter Ali Octopizzo amesema aliamua kuweka kando kila kitu kwa ajili ya afya yake ya akili lakini pia kujihusisha na mambo ambayo yataamuingizia hela kwani alikuja kugundua kuwa alikuwa anapoteza muda wake mwingi kupishana na watu wasiokuwa na malengo maishani.

Octopizzo ambaye anafanya vizuri na ngoma mpya “Tom Mboya” amesema kwamba anapenda sana watu wanapomkosoa mtandaoni kwa kuwa inampa changamoto ya kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo haviendi sawa kwenye muziki wake.

Utakumbuka Octopizzo amekuwa kwenye tour yake tangu mwezi Machi Mwaka huu ambapo amekuwa akihubiri amani na kuwahamasisha vijana wajitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi watakaowafaa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke