Rapa Octopizzo amewahimiza wasanii wakubwa Afrika Mashariki kuhakikisha wanaisaidia jamii kwa kuwawezesha watu wenye uhitaji.
Akizungumza katika mahojiano na Wasafi, Octo ameeleza kuwa hapendi kila kitu kuhusu msanii Diamond ila anafarajika na namna ambavyo ametengeneza fursa za ajira kwa vijana.
Octopizzo pia amewatolea uvivu wasanii ambao hutumia kiki kutangaza muziki wao kwa kusema kwamba wana njaa ya maskini.
Rapa huyo amewataka wasanii nchini Kenya kuzingatia suala la kutayarisha muziki mzuri badala ya kiki ambazo hazina msingi wowote.
Hata hivyo amesema kwamba haihitaji kuimba Kiingereza ili utoboe kimataifa, kwani kuna ngoma nyingi sana zimekuwa kubwa dunia nzima na hazijaimbwa kwa Kiingereza.