You are currently viewing OCTOPIZZO AWEKA WAZI VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

OCTOPIZZO AWEKA WAZI VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

Rapa Octopizzo  amefunguka kuhusiana na swala la yeye kutofanya kolabo na wasanii wenzake hususani wa nje.

Kupitia Mambo Mseto ya Radio Citizen Octopizzo amesema hatokuja kufanya kolabo na mtu ambaye ana faida kwake kwa kuwa anafanya muziki kama biashara.

Haikushia hapo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba ikitokea amefanya kolabo na msanii yeyote ni lazima awe na Master Recording za muziki wake kwani hapendi suala la kufaidisha lebo za muziki.

Mbali na hayo ameonyosha maelezo kuhusu kufanya wimbo wa pamoja na Khaligraph Jones kwa kusema watafanya kazi na rapa huyo muda sahihi ukifika kwa kuwa hawana ugomvi kama walimwengu wanavyodai mtandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke