You are currently viewing OCTOPIZZO KUKATA KIU YA MASHABIKI NA MOTIVATION ALBUM

OCTOPIZZO KUKATA KIU YA MASHABIKI NA MOTIVATION ALBUM

Staa wa muziki wa hiphop nchini  Octopizzo ametangaza kuachia album yake mpya  inayokwenda kwa jina la “Motivation”

Octopizzo ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akiwawataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea album hiyo ambayo kwa mujibu wake ipo njiani.

Hitmaker huyo wa “Babylon” amesema  mashabiki wanaweza kui-pre-order kupitia majukwaa ya muziki kama Spotify na Apple music ila tayari ameachia ngoma ya kwanza kutoka kwenye album hiyo iitwayo “Motivation”.

Motivation  itakuwa ni album ya sita kwa mtu mzima Octopizzo baada ya Jungle Fever iliyotoka mwaka wa 2020 ikiwa na jumla ya mikwaju 15 ya moto.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke