You are currently viewing OCTOPIZZO KUWANIA TUZO ZA GRAMMY 2022

OCTOPIZZO KUWANIA TUZO ZA GRAMMY 2022

Habari nzuri na kubwa kwa muziki wa Kenya ni kuwa , Kwa mara ya pili  staa wa muziki nchini Octopizzo amefanikiwa kuingia kwenye hatua ya kujadiliwa yaani Consideration kwa ajili ya kuingia kuwania Tuzo za Grammy mwaka wa 2022.

Kwa mujibu wa Grammy Awards Academy wamempendekeza mkali huyo kutoka Kenya katika vipengele vinne ambavyo ni Best Global Album kupitia album yake ya Jungle Fever), Best Global music performance kupitia ngoma ya “Lela”, Best Rap Song  na Best Rap Performance kupitia ngoma yake ya Pockets na Interlude.

Octopizzo ameshare habari hii njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kipindi ataleta tuzo za Grammy Kibera sehemu ambayo amekulia tangu utotoni.

Hata Hivyo Octopizzo anaungana na baadhi ya wasanii wengine duniani kusubiri kura za mapendekezo kutoka Academy ya Grammy , na akipitishwa basi wataingia Moja kwa moja kuwania tuzo hizi zenye heshima kubwa Ulimwenguni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke