You are currently viewing ODI WA MURANG’A AMCHANA VDJ JONES KISA EDU MADOXX WA BOONDOCKS GANG

ODI WA MURANG’A AMCHANA VDJ JONES KISA EDU MADOXX WA BOONDOCKS GANG

Msanii Odi wa Murang’a amemtolea uvivu VDJ Jones baada ya DJ huyo kudai kuwa msanii wa Boondocks Gang Edu Madoxx alizembea kwenye muziki kutokana na kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Katika mahojiano na Mungai Eve Amemtaka VDJ Jones aache suala la kutumia stori ya Edu Madoxx kujitafutia kiki na badala yake ajishughulisha na mambo yatakayomsaidia maishani kwani angekuwa mtu mwema angekuwa amewasaidia wasanii wanaothirika na dawa za kulevya.

Lakini pia hajamzaza msanii wa Sailors Gangs Cocos Juma kwa kuhoji kuwa mbona hakuzungumza masaibu yake na lebo ya Black Market Records kabla Maddox hajaweka wazi stori yake akiwa chini ya Boondocks gang ambapo ameenda mbali Zaidi na kusema kwamba Cocos Juma sio msanii kwani watu wanafahamu kama mtu wa kupiga mayowe.

Kauli ya Odi wa Murang’a mara baada ya yeye pamoja na msanii Exray kujitokeza na kukanusha madai ya kumtelekeza Edu Maddox katika kundi la Boondocks Gangs.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke