You are currently viewing OFFSET AISHTAKI LEBO YA QUALITY CONTROL MUSIC

OFFSET AISHTAKI LEBO YA QUALITY CONTROL MUSIC

Rapa Offset ameifungulia mashtaka label yake (Quality Control Group) kwa kukiuka makubaliano ambayo waliingia January mwaka 2021.

Kwa mujibu wa TMZ Hip Hop, Offset alifungua shauri hilo Jana Jumanne akisema aliingia makubaliano na label hiyo, ya ufanyaji kazi za peke yake (solo deal) na alilipa pesa nzuri tu kwa ajili ya kupata haki zake kama Solo Artist.

Sasa baada ya kuachia ngoma yake mpya “5 4 3 2 1” chini ya Universal Music Group, Offset anadai kwamba Quality Control Group wanajaribu kutaka kuwa wamiliki wa kazi hiyo, kitendo ambacho amekiita chuki. Kwa sasa QC wanafanya kazi na Offset kwenye makubaliano ya kundi pekee ambalo ni Migos.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke