Rapa kutoka Marekani Offset ametoa heshima kwa marehemu Virgil Abloh ambaye alikuwa ni rafiki yake lakini pia Mshirika wake Kibiashara, kwa kuchora Tattoo yenye sura yake, ametuonesha kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram.
Offset sio wa kwanza kufanya hivyo, Drake pia ni miongoni mwa wasanii wenye Tattoo ya Virgil Abloh ambaye alifariki November 28, 2021 kwa ugonjwa wa Saratani.
Virgil Abloh alikuwa mwanamitindo maarufu nchini Marekani na Mkurugenzi wa Sanaa upande wa mavazi ya Kiume katika kampuni ya Louis Vuitton, pia mmiliki wa Kampuni ya Off-White.