Msanii wa HipHop nchini Ohms Law Montana amefichua kuwa watu wa karibu na gavana Ali Hassan Joho ndio waliosambaratisha safari yake ya kuenda nchini Marekani hata baada ya Gavana huyo kumkatia tiketi ya kuelekea nchini Marekani.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Ohms Law Montana amesema Gavana Joho aligharamia nauli yake ya usafari ila hakupewa tiketi hizo na watu wa karibu na gavana huyo.
Aidha Ohms Law Montana amesema kuwa hajuitii kukosa safari hiyo huku akisema hatua hiyo inaendela kumpa msukumo wa kuendeleza vuguvugu lake la Acha Gun Shika Mic ambalo kwa sasa amefichua imepata udhamini kutoka kwa shirika moja nchini Uingereza.
Hata hivyo rapa huyo amesema kwa sasa hafanyi video za muziki ila anawekeza sana kufanya Documentaries ambazo amesema zimempa nafasi kubwa ya kuweza kukutana na watu wenye ushawishi mkubwa duniani waliojitolea kuisadia vuguvugu lake la Acha Gun Shika Mic