Mwanamuziki kutoka Kenya Okello Max ameachia rasmi Album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Album hiyo inakwenda kwa jina la Boss ina jumla ya nyimbo 15 na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Bassman, Bonysun, Suzanna Owiyo, Femi One, Bien Bensoul, Coster Ojwang’, Jocelina, Charisma na Watendawili.
Boss Album ina nyimbo kama Pull Up, Nipe Nafasi, Kuwa na Wewe, Kungfu,Boss Oreo na nyingine nyingi.
Boss ni Album ya kwanza kwa mtu mzima Okello Max tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay.