You are currently viewing OLE GUNNAR ATIMULIWA MAN UNITED

OLE GUNNAR ATIMULIWA MAN UNITED

Hatimaye klabu ya Manchester United imefanya maamuzi ya kuachana na kocha wake Ole Gunnar Solskjaer baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha kushtukiza cha mabao 4-1, kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana Jumamosi.

Kwa mujibu wa Sky Sports, baada ya kipigo hicho cha kushtua, bodi ya Man United iliitisha kikao cha dharura kujadili hatima ya Solskjaer ambapo bodi hiyo ilifika makubaliano ya Solskjaer kutimuliwa kazi haraka iwezekanavyo.

Kiungo wa zamani wa Klabu hiyo Michael Carrick ametajwa kushika mikoba ya Ole kwa michezo inayofuata wakati Klabu ikitazamia kuteua Kocha wa muda mpaka mwisho wa msimu.

Man United imefungwa mechi saba katika mechi 13 walizocheza msimu huu, rekodi mbovu chini ya kocha huyo raia wa Norway.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke